kufuru kubwa za mayweather
Ulishawahi kujiuliza kwamba maisha yatakuaje kama ungekua na utajiri wa Bilioni 900 za kitanzania.? Fikiria umeipata hicho kiwango kwa siku moja au kwa kujumuisha miaka yako yote..utazitumiaje pesa zako? Utafanya nini? Watu wanasema kwamba unapotengeneza pesa zaidi ndipo matatizo mengi unayatengeneza ambayo utakumbana nayo, lakini embu tuangalie ukweli, kukaa karibu na mabilioni cash ni mojawapo ya tatizo zuri kupata. Floyd Mayweather anafanya kazi kwa bidii sana na si ajabu katika hilo, huwezi ukafika kilele cha mafanikio yako katika michezo bila kutoa maisha yako yote kua bora duniani. Mayweather tangu udogoni alikua commited katika mazoezi na kujifunza mchezo wa masumbwi na ni sababu yuko katika hio nafasi aliyopo leo hii, mwanamichezo anayelipwa pesa nyingi duniani. Umchukie au umpemde jamaa ananuka utajiri na mafanikio, lazima tukubali anajua jinsi gani ya kula matunda ya jasho lake, kuna siku aliingia duka la nguo na viatu akawanunulia wadada wote waliokuepo vitu walivyohitaji sasa sjui waliokua na wenza wao walijisikiaje anyway chini hapo ni manunuzi 12 makubwa kati ya manunuzi ghali aliyowahi kufanya hadi hivi sasa. Basi dogo la kufanyia party ndani Basi hili alilinua kwa shilingi bilioni 1.3, humo ndani kuna viti vya kufanyiwa massage, bar ya kujitosheleza, satellite tv, na system ya nguvu, hili lilitengenezwa kwa order maalumu. BestChauffeured-SprinterMercedesInterior.jpg Mabegi ya nguo ya Hermes Floyd_Mayweather_hermes_bags.jpg Alinunua mabegi haya Paris Ufaransa, kwenye duka moja kwa shilingi milioni 900 Alinunua Mkataba shutterstock_273788027-1.jpg Alitaka kua na kampuni yake mwenyewe kwahio akaona isiwe shida anunue mkataba aliokua nao na kampuni ya Toprank Promotions..wazo hili ndilo limemfanya awekeze nguvu nyingi katika kampuni yake na kumfanya kua mwanamichezo anayelipwa hela nyingi. Alinunua mkataba huo kwa shilingi bilioni 1.6. Kumfanyia mtoto wake sherehe ya kuzaliwa Alimfanyia mwanawe wa miaka 16 birthday party ambayo ilikua private ambapo Drake na Future waliitwa kuja kutumbuiza. Alilipa private party hio shilingi Bilioni 2. shutterstock_59022472.jpg Saa ya gharama Alinunua saa hii aina ya Hublot chini Dubai kwa shilingi Bilioni 2.4 hublots-big-bang-10-years-haute-joaillerie-is-a-millions-dollar-game-video-93653_1.jpg Kubeti Mayweather anapenda sana kubeti ...unaweza kuona ni ukichaa lakini ni kweli alibeti kwenye kamari ya mchezo mmoja bilioni 2.4 lakini ajabu alishinda. BBjcBJI.img_.jpeg Jumba la thamani floyd.mayweather.home_.16-1.jpg Mayweather amemunua jumba hili kwa shilingi bilioni 3.3 Gari la kifahari aina ya Buggati Floyd-Mayweather-Bugatti.jpg Sidhani kama kuna gari la thamani kubwa duniani ambalo hana, alinunua gari hili lenye thamani kwa shilingi bilioni 7.8 Kuweka tu vitu sawa hapa, marekebisho madogo(service) na mafuta katika hili gari ni shilingi milioni 45. Gari lingine la kifahari. Amenunua gari hili kwa shilingi bilioni 10. m5.jpg Jumba lingine la kifahari. Jumba hili lenye vyumba vitano vya nguvu na mabafu 7 liko Las Vegas Marekani, amelinunua kwa shilingi bilioni 20. Unaambiwa hapa anawalipa watunza bustani shilingi milioni 6.5 kwa mwezi kwa kutunza tu bustani yake ya maua, fensi na miti. Floyd-Mayweather-Car-Collection-01.jpg Pete ya UCHUMBA kwa mpenzi wake Kuna msemo maarufu unasema "diamonds are forever" , pete hii ya uchumba alimnunulia mpenzi wake Shantel Jackson,ambapo aliinua kwa shilingi bilioni 22, na alikua pia akimnunulia zawadi mbalimbali kama magari, na vito vya thamani lakini mwaka 2013 alipokaribia kumchumbia mpenzi wake huyo ghafla alivunja uchumba na kusitisha sherehe za kumchumbia kwa kumvalisha pete hio sababu aligundua alitoa mimba yake bila yeye Mayweather kujua. 333ad6c4ea9f29c9564af345844ccd3f.jpg Ndege binafsi Sio ajabu kumkuta wiki hii yuko Cairo, wiki ijayo yuko Dubai, wiki inayofata yuko Paris..ukiwa na private jet yako hupati shida ya kusafiri nchi yoyote duniani kwa muda wako,unachagua tu wapi unataka kwenda. Alinunua kwa shilingi bilioni 78. Kwa haraka haraka katumia zaidi ya Bilioni 150 kwa vitu hivi tu, hatujui na mengine.

0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home