NEWS/EDUCATION & TRICKS
Friday, February 9, 2018
Tuesday, February 6, 2018
FID Q AMTANGAZA RASMI MCHUMBA WAKE
Mkali wa HipHop Bongo Fid Q ameonekana kukamatika kimahaba kwa mrembo ambaye amemtambulisha nyumbani kwao Mwanza na ameiambia eNEWZ kuwa kwa sasa yupo kwenye mahusiano rasmi. Fid Q amesema ameamua kupost picha kwenye mitandao yake ya kijamii ili kupunguza wasichana wengine kumtumia meseji za kumsumbua lakini pia kuwaonyesha mashabiki zake kwamba kwa sasa yupo katika mahusiano rasmi kwani umri wake unaruhusu. ''Nimeamua kuweka mahusiano yangu wazi ili kuzuia usumbufu wa kina dada wanaonisumbua katika mitandao ya kijamii na hata ninapokuwa kwenye viwanja vya starehe na mda wowote kuanzia sasa ninaweza kutangaza ndoa'', amefunguka
Monday, February 5, 2018
TUNDA SEBASITA AWEKEWA KIKAO CHA DHARULA
DAR ES SALAAM: Kufuatia sakata la video akiwa anafanya vitendo vya kimahaba na mume wa mtu, Kinjekitile Kingunge ‘Kinje’ kusambaa mitandaoni hivi karibuni, muuza sura katika video mbalimbali za wasanii wa muziki Bongo, Tunda Sebastian amejikuta akiwekwa kitimoto na familia yake. Uchunguzi wa gazeti hili kupitia kwa rafiki wa karibu na Tunda ulionesha kwamba baada ya video hiyo kusambaa ilikuwa ni patashika nguo kuchanika kwani wazazi wake walikasirishwa mno na kitendo hicho, ndipo wakamweka kitimoto japokuwa hadi sasa hajakaa nao sawa. “Familia ya Tunda ilimweka kitimoto mwanadada huyo na kumsema sana ambapo aliahidi kwamba atabadilika na akawaangukia wazazi wake na kuwaomba msamaha licha ya kuwa haikuwa kazi rahisi kwa kweli,” alisema rafiki huyo. Ijumaa Wikienda lilimtafuta Tunda ambaye alieleza kuwa, baada ya video hiyo kuvuja kulitokea mtafaruku mkubwa kwa wazazi wake huku mpenzi wake akikasirishwa na kitendo hicho na hadi sasa hazungumzi naye. “Nimejifunza sana maana ile video imenivuruga sana kwa kweli kwani wazazi wangu walikasirika sana, mpenzi wangu mpaka sasa haongei na mimi ila bado ninaendelea kumwelewesha kwamba ile ilikuwa ni pombe tu. “Naamini hasira zake zikiisha atanitafuta tu maana najua ananipenda, nimekoma kunywa pombe na nimeshaacha kabisa kwa kweli,” alisema Tunda. Video hizo zilikuwa gumzo mitandaoni kabla ya Kinje kufiwa na baba yake, Mzee Kingunge hivyo watu kuacha suala hilo kwani ni kumuongezea maumivu juu ya maumivu. Muungwana
DONAD TRUMP AMKATAZA MARADONA KUINGIA MAREKANI
Rais wa Marekani Donald Trump ameripotiwa kumpiga marufuku mchezaji wa zamani wa Argentina na mshindi wa Kombe la Dunia, Diego Maradona kuingia nchini Marekani. Mwanasheria wa mwanasoka huyo wa zamani amesema kuwa Maradona hatohudhuria kesi yake jijini Miami kutokana na nyota huyo kuzuiwa na Rais Trump kwa madai kuwa alitoa lugha ya kashfa kwa Trump kwenye mahojiano na Television nchini Venezuela. ''Maradona hatoweza kuwepo kwenye kesi yake dhidi ya mke wake wa zamani kwasababu amezuiwa na Rais Trump'', amesema Mwanasheria huyo. Muargentina huyo alihitajika kusafiri wiki hii kwenda Miami, Florida, kwenye kesi yake dhidi ya mke wake wa zamani Claudia Villafane, ambaye anamshitaki kwa kumuibia fedha na kununua mali mbalimbali nchini Marekani. Maradona anakumbukwa kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 1994 nchini Marekani, akiwa nahodha wa Argentina alirudishwa nyumbani baada ya kupimwa na kugundulika ametumia madawa ya kulevya aina ya Cocaine.
HISTORIA YA YANGA (Young africans sport club)
yanga ilianzishwa mnamo mwaka 1935 na inasemekana ndo klabu kongwe na yenye mafanikio zaidi hapa nchini. klabu hii ilianzishwa na wazalendo halisi wa nchi hii waliokuwa wakiji shughulisha na uchuuzi wa nazi na samaki na muda wao wa jioni ulipofika walikuwa wakijumuika pamoja kusakata kabumbu na hapo ndipo ilizaliwa yanga. kama hiyo haitoshi wazalendo hawa waliendelea kujikusanya kwa pamoja na kuanza mishemishe za kusaka uhuru wa nchi hii, na ndipo tarehe 9 disemba mwaka 1961 tanganyika ikapata uhuru, hivyo kama tutazungumzia uhuru wa taifa hili basi hatusiti kwa namna moja au nyingine kuitaja yanga, na kwa heshima yake inatakiwa unapoitaja yanga kama umekaa basi unatakiwa usimame. MAFANIKIO. yanga ndio timu iliyochukua ubingwa wa ligi ya bara mara nyingi zaidi, na ndio klabu inayofahamika zaidi kitaifa na kimataifa kwa sababu ndiyo klabu iliyopeperusha vizuri bendela ya taifa hili la tanzania nje ya mipaka. na kama hiyo haitoshi yanga ndiyo klabu yenye washabiki wengi zaidi ndani na nje ya nchi, ndani ya africa na dunia kwa ujumla. na pia yanga ndiyo klabu ya mwanzo hapa nchini au hata afrika mashariki kwa ujumla kwa kuwa na makao makuu sambamba na uwanja wa mazoezi ambao unajulikana kwa jina la Kaunda, jina la muasisi na mpigania uhuru mwengine wa taifa la zambia muheshimiwa keneth kaunda. mfumo huu wa kuwa na makao makuu pamoja na uwanja wa mazoezi ni wa timu kubwa barani ulaya na dunia kwa ujumla. yanga pia ndio timu ya kwanza kuwa na gazeti hapa nchini. gazeti hili linajulikana kama "Yanga imara". lilipotoka katika wiki ya kwanza liliuzwa takriban nakala 50,000 nchi nzima na baadhi ya nchi za jirani. mfumo wa kuwa na gazeti la klabu pia umeigwa na baadhi ya klabu hapa nchini lakini unaonekana kusua sua katika mauzo na hata ukisoma nakala ya gazeti lao utakuta limejaa matangazo ya waganga tu. yanga ndo timu pekee iliyowahi kuuza mchezaji nje ya nchi na kung'aa katika vilabu mbali mbali barani ulaya, mchezaji huyu alijulikana kama Nonda Shaaban al maarufu kama "papii". nonda ambaye aliwahi kutamba na mashujaa hawa wa jangwani amepata kuchezea vilabu kama val profesional ya south africa, FC zuurich ya uswis, stade rennes na AS monaco zote za ufaransa, AS roma ya italia akicheza pamoja na francesco totti, blackburn ya uingereza na sasa anakipiga katika klabu ya galatasaray yenye maskani yake katika uwanja wa ali sami yen nchini uturuki. na hapa ndipo tunapoitofautisha yanga na vilabu vingine vya soka hapa nchini ambavyo wachezaji wake huuzwa burundi, rwanda na uarabuni ambako hakuna soka la ushindani. pia yanga ndo timu ya kwanza hapa nchini kuongozwa na rais. pia yanga ndo timu ya kwanza kuwa na mfumo wa wanachama kuwa wana hisa wa klabu kama timu nyingi za ulaya, hivyo kumfanya kila mwanachama kuhusika kikamilifu katika mipango na malengo ya klabu, tofauti na majirani zetu ambao mfumo wao wa uongozi haueleweki na hata mishahara ya wachezaji wanalipwa kimkanda mkanda na inafika kipindi mchezaji anakaa miezi minne hajalipwa mshahara mwisho wanatimkia kucheza ligi za mchangani. MAFANIKIO NJE YA MIPAKA. Yanga kama yanga ndo timu pekee iliyowahi kuchukua kombe linalotambuliwa na shirikisho la soka barani afrika CAF na shirikisho la soka duniani FIFA. itakumbukwa tu yanga waliwafunga express ya uganda kwa goli 3-1 katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la klabu bingwa afrika mashariki na kati na mechi ya fainali walitakiwa wakipige na SC villa. yanga waliwacharaza bila huruma SC Villa goli 2-1 katika uwanja wa nakivubo kwenye mechi ya fainali ya kombe lililokuwa na msisimko kipindi hicho la klabu bingwa afrika mashariki na kati na kupelekea serikali ya tanzania kutuma ndege mpaka katika uwanja wa ndege wa entebe kwenda kuwachukua waheshimiwa waliolitoa taifa kimasomaso yaani yanga. hivyo kuweka adabu kwa waganda ambao hawawezi kuisahau yanga maishani mwao. yanga katika mechi hiyo iliwakilishwa na: 1) steven nemes 2) mwanamtwa kihwelu 3) keneth mkapa 4) willy mtendamema 5) issa athuman 6) method mogella 7) steven mussa 8) hamis thobias gagarino 9) said mwamba kizota 10) mohamed husein chinga one 11) edibily jonas lunyamila pia yanga walikuwa na bunduki nje kwenye benchi kama willy martin, rifat said, aboubakar salum "sure boy" david mwakalebela "MP" na wengine wengi ambao walikuwa ni miiba kwa waganda. katika mechi hiyo mnamo dakika ya 81 beki mahili wa villa na timu ya taifa ya uganda marehemu Paul Hasule alivua jezi na kutoka nje kwa kile ambacho mwenyewe alikiri kuwa ameshindwa kumkaba winga wa yanga edibily lunyamila, lakini alilazimishwa na kocha wake kumaliza mechi kutokana na aibu iliyokuwa inawakabili. kutokea hapo waganda walitekwa akili kutokana na kabumbu safi lililoonyeshwa na yanga na kupelekea daladala nyingi nchini humo kuandikwa majina kama "lunyamila trans" "kizota trans" au hata wengine walifuta majina ya salon zao na kuandika "gagarino hair salon" na mpaka leo hii waganda wakisikia timu kutoka tanzania inakwenda huko wanauliza "je ni yanga?". na baada ya ushindi huo mwanamuziki nguli wa afrika marehemu kabasele yampanya al maarufu kama peppe kalle alitunga wimbo wa kuisifia timu hiyo baada ya kuonyesha dhahili kiwango cha juu na kuvutia washabiki wengi wa soka kitu ambacho hakijawahi kufanywa na klabu yoyote nyingine hapa nchini. HISTORIA ISIYO SAHAULIKA. mwaka 1972 katika pambano la watani wa jadi lililokuwa lifanyike katika uwanja wa taifa, watanzania walishuhudia kituko cha mwaka pale kilabu ya simba ya dar es salaam ilipoishia chang'ombe na kugeuza basi na kurudi katika mtaa wa msimbazi na kufanya timu ya yanga ya tanzania kupewa ushindi baada ya mpinzani kufyata mkia na kutokomea vichakani. mnamo pia tarehe 13 mwezi novemba mwaka 1991 katika uwanja huo huo wa taifa timu ya yanga ya tanzania waliingia uwanjani na basi la sharuksi lililokuwa likimilikiwa na mfadhili wa yanga wa kipindi hicho marehemu abbas gulamali, timu ya soka ya simba ya dar es salaam iliweka mpira kwapani wakati wa mapumziko na kutokomea kusiko julikana. na kauli hii ya kuweka mpira kwapani iltolewa na mtangazaji aliyekuwa anatangaza soka redio tanzania siku hiyo ndugu Charles Hillary, na magazeti kama motomoto, mfanyakazi, uhuru na mzalendo ya kipindi hicho yalipambwa na kichwa kikubwa cha habari "mgonjwa atema dawa". na kuweka mpira huko kwapani kulifuatia vipigo mfululizo vya august 31, october 9 lakini hii iltanguliwa na kipigo cha Said Sued "Scud" cha mei 18. baadhi ya mashujaa waliowahi kukipiga yanga miongoni mwao ni rifat said, joseph katuba, peter manyika, anwar awadh, salum kabunda "ninja", godwin aswile "baba subi" au scania, said zimbwe, thomas kipese, joseph lazaro, omar husein, costantino kimanda, sanifu lazaro "tingisha" na wengine wengi. hili nililokupa hapo ni tone tu la maji, ila bahari ntakupa siku nyingine. na hii ndo yanga, klabu bora kabisa hapa nchini, isiyotishwa na kelele, adhabu wala faini yoyote.
DIAMOND APATA SKENDO NYINGINE TENA
Mwanamuziki aliyeuteka ulimwengu wa Bongo fleva Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amejikuta ndani ya skendo nyingine baada ya mwanadada mrembo anayeitwa Mia kukiri kuwa alilala na nae nyumbani kwake Madale. Wiki chache zilizopita Diamond alikamata headlines zote kwenye mitandao ya kijamii baada ya msichana huyo aliyetambulika kwa jina la Mia kuonekana akijirekodi ndani ya nyumba ya Diamond iliyoko Madale. Baada ya kusambaa kwa video hiyo, mara moja taarifa zilienea kuwa msichana huyo alikuwa ni mchepuko wa Diamond na alikwenda Madale, jambo ambalo lilizua tafrani hata kwa Zari ambaye aliamua kumrushia dongo na kusema Madale pamekuwa Guest house. Lakini tetesi hizo zilizimwa siku inayofuata baada ya timu ya Diamond kusambaza picha na video zilizokuwa zinamuonyesha msichana yule akiwa nyumbani kwa Diamoand, Madale lakini safari hii alionekana akiwa amekumbatiana na Bajuni ambaye ni mmoja Kati ya madansa wa WCB. Hivyo kuonekana kuwa Mia alikuwa ana uhusiano na Bajuni na sio Diamond kama ilivyodaiwa awali. Ikiwa ni wiki chache tu zimepita baada ya sakata hilo kutokea, mrembo Mia amefunguka na kueleza ukweli wote ambapo amedai kuwa habari zilizoenezwa kwenye mitandao ya kijamii sio za kweli kwani yeye alienda Madale kumfuata Diamond. Katika mahojiano aliyofanya na kipindi cha Shilawadu kinachorushwa na runinga ya Clouds, Mia alifunguka na kusema kuwa, alipigiwa Simu na Diamond aende Madale mida ya saa nne usiku na alipofika akalala naye mpaka asubuhi ya kesho yake asubuhi ndipo alichukua simu yake akajirekodi video akiwa anatembea tembea nyumbani hapo. Kwa mujibu wa maelezo ya Mia, Diamond alimuona akijirekodi kupitia kamera zilizokuwa mule ndani, ndipo akaichukua simu yake kwa lazima na kuanza kuisachi, kisha akaifuta kila kitu kilichokuwepo yaani picha zote mpaka video. Aliendelea kueleza kuwa, baada ya hapo Diamond akawaita Bajuni na Harmonize na wakamlazimisha aanze kupiga picha na Bajuni ili ionekane kama ni wapenzi ili baadaye Diamond aje aseme alienda Madale kwa Bajuni na siyo kwake. Mia aliongea kwa uchungu akidai amedhalilishwa na Diamond na watu wote wamejua kuwa yeye anatembea na Bajuni wakati alikuwa hajawahi hata kumuona hapo kabla wakati aliyeenda kumfuata Madale ni mwenyewe Diamond Muungwana
PADRE AMZIKA MOZEY RADIO KWA MAJUNGU
Padri aliyeendesha misa ya kumuaga marehemu #MowzeyRadioaitwae Katerega Kiibi jana kaendesha misa vizuri. Nilichopenda kutoka kwake aliongea ukweli wote bila kuficha kitu mbele ya kadamnasi. Alisema kuwa wasanii inabidi waache kutumia Vilevi vya aina yoyote, Waache kuishi maisha ya anasa, waache kuwatelekeza wake zao na waache kabisa kujihusisha na ugomvi usio wa lazima. Kaenda mbali na kudai kuwa watu wanapokuwa maarufu wananza kuishi maisha ya kiovu na kuwa na tabia mbaya. Hakuishia hapo aliwapa na ushauri pia kuwa wasitumie pesa vibaya, wajifunze namna ya kuitumia. Wajifunze namna ya ku handle umaarufu. Aliongezea: kwanini huwezi kuwa na matumizi mazuri ya pesa unayoingiza ukazuia watu wasiandae harambee ya kukuchangua wakati ulifanya kazi zaidi ya miaka 20 na uliingiza hela nyingi?? NENO MOJA KWA MCHUNGAJI HUYU TAFADHALI Source :instagram











