FID Q AMTANGAZA RASMI MCHUMBA WAKE
Mkali wa HipHop Bongo Fid Q ameonekana kukamatika kimahaba kwa mrembo ambaye amemtambulisha nyumbani kwao Mwanza na ameiambia eNEWZ kuwa kwa sasa yupo kwenye mahusiano rasmi. Fid Q amesema ameamua kupost picha kwenye mitandao yake ya kijamii ili kupunguza wasichana wengine kumtumia meseji za kumsumbua lakini pia kuwaonyesha mashabiki zake kwamba kwa sasa yupo katika mahusiano rasmi kwani umri wake unaruhusu. ''Nimeamua kuweka mahusiano yangu wazi ili kuzuia usumbufu wa kina dada wanaonisumbua katika mitandao ya kijamii na hata ninapokuwa kwenye viwanja vya starehe na mda wowote kuanzia sasa ninaweza kutangaza ndoa'', amefunguka


0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home